HabariMilele FmSwahili

Gavana Obado ahojiwa wakati huu na maafisa wa DCI Kisumu

Gavana wa Migori Okoth Obado anahojiwa wakati huu na makachero wa idara ya jinai DCI mjini Kisumu. gavana Obado alijiwasilisha katika makao makuu ya DCI mjini humo saa nne asubuhi. Haijaarifiwa atakachohitajika kuelezea hata hivyo obado anahojiwa kufuatia shinikizo kutoka kwa viongozi mbali mbali wa kisiasa wakimtaka kuwajibikia mauaji ya Sharon Otieno aliyekuwa mwanafunzi  wa chuo kikuu cha Rongo kaunti ya Migori. Hata hivyo gavana  Obado tayari amejitenga na mauaji hayo huku akiwataka polisi kuendesha uchunguzi wa kisa na kubaini waliohusika pamoja na kiini chake. Kando na Obado mwanahabari wa Nation Barrack Oduor pia amehojiwa na maafisa wa DCI mjini Kisumu. Kati ya mengine polisi wamemtaka Barrack kuwasilisha nguo alizokuwa amevaa wakati wa utekaji nyara wake.

Show More

Related Articles