HabariMilele FmSwahili

IEBC kutumia vifaa na mashine ilivyotumia 2017 katika uchaguzi wa 2022

Tume ya IEBC itatumia vifaa na mashine ilivyotumia wakati wa uchaguzi wa mwaka 2017 katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022. Mwenyekiti Wafula Chebukati anasema hii itasaidia kupunguza gharama ya kuandaa  chaguzi nchini. Akizungumza katika mkao na wadau pamoja na wafadhili waliosaidia IEBC uchaguzi uliopita, Chebukati anasema ipo wameweka mikakati mahususi kuzuia uharibifu wa fedha kama ulivyoshuhudiwa katika uchaguzi uliopita.Chebukati pia anasema msasa wa wafanyakazi wa IEBC utaandaliwa kuhakikisha wanaohudumu wanaaminika.Wakati huo Chebukati ameituhumu wizara ya fedha kwa kuzuia kuwepo hazina ya fedha ya IEBC, hali inasema imewazuia kuwalipa wanaoidai IEBC

Show More

Related Articles