HabariMilele FmSwahili

Mwanaume wa miaka 48 auwawa kufuatia mzozo wa ardhi Nyeri

Mwanaume wa miaka 48 ameuwawa kufutia mzozo wa ardhi katika kaunti ya Nyeri. Inaarifiwa jamaa huyo ameuwawa na  kakake mdogo usiku wa kuamkia leo  kufuatia mzozo baina yao nyumbani kwao katika kijiji cha Giteru eneo bunge la Nyeri. Mwenyekiti wa mpango sera za jamii kuhusu usalama James Wambugu anasema wawili hao wamekuwa wakizozania umiliki wa ardhi hiyo kwa muda mrefu.

Show More

Related Articles