HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta kukutana na maafisa wakuu wa wizara ya fedha leo

Rais Uhuru Kenyatta atakutana na maafisa wakuu wa wizara ya fedha na uongozi wa bunge hii leo kujadili hatima ya utekelezwaji wa sheria ya ushuru wa asilimia 16 kwa bidhaa za mafuta.Inaarifiwa rais amekuwa akishauriana na wadau kabla ya kuamua iwapo atasaini  msuada wa kuhairisha utekelezwaji wa sheria hiyo  kwa 2 miaka. Mkutano wa leo utahusdhuriwa na waziri wa fedha Henry Rotich, spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi miongoni mwa viongozi wengine. Inakisiwa rais analenga kufanya maamuzi mawili aidha kupendekeza kupunguzwa ushuru huo kutoka asilimia 16 hadi asilimia 10 au afutilie mbali baadhi ya miradi ilionuiwa kufadhiliwa na ushuru huo.  Japo wamekana kuangazia utata huo,wabunge wanachama wa kamati ya bajeti bungeni wanakutana Mombasa wakiripotiwa kusaka mwafaka kuhusu sheria hiyo,.

Show More

Related Articles