HabariPilipili FmPilipili FM News

Washukiwa 3 Wa Uhalifu Watiwa Mbaroni Katika Kaunti Ya Mombasa.

Maafisa wa polisi kaunti ya Mombasa wamewatia mbaroni washukiwa watatu wa uhalifu ambao wanadaiwa  kuwahangaisha wananchi kaunti ya Mombasa katika eneo la mwembe tayari usiku wa jumapili na usiku wa jana mtawalia.

Akiongea na wanahabari kamanda wa polisi kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara anasema washukiwa hao walikamatwa wakiwa na silaha walizo kua wakizitumia kutekeleza uhalifu huo.

Aidha anasema polisi wataendelea kuwazuilia washukiwa hao ili kuwasaidia  katika oparesheni yao ya kuwakamata wahalifu zaidi.

 

Show More

Related Articles