HabariPilipili FmPilipili FM News

Visa Vya Waraibu Wa Mihadharati Kuuawa Vimepungua Katika Kaunti Ya Kwale.

Huku ulimwengu ukiadhimisha  siku ya kuepukana na kujitia kitanzi almaarufu world suicide day,visa vya waraibu wa utumizi wa dawa za kulevya kuuwawa  kaunti ya kwale  vimepungua tangu serikali  kuanzisha mpango wa kuwapatia waraibu dawa za kupunguza makali almaarufu methadone.

Zaidi ya vijana 20 ambao ni waraibu   wa  dawa  za  kulevya  wameuwawa katika eneo la Diani kwa kushukiwa kijihusisha na wizi mdogo mdogo huku wengine wakisalia na makovu kutokana na wizi waliokua wakitekeleza.

Kulingana na Ahmed Ali  afisaa  wa  kituo cha kurekebishia tabia  cha teenswatch huko Ukunda  amesema kuwa  watumizi wa mihadarati  walijiingiza katika jinamizi hilo  kutokana na msongo wa mawazo

Show More

Related Articles