HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakaazi Wa kwale Wapinga Vikali Hatua Ya Idara Ya Usalama Kuagiza Kufungwa Kwa Vibanda Vya Kuonesha Video.

Baadhi ya wakaazi wa eneo la Msambweni  kaunti ya Kwale wanapinga vikali hatua ya idara ya usalama  kaunti  hio kutaka kufunga mabanda yote ya video kwa tuhuma kuwa mabanda hayo huonesha  sinema za ngono kwa watoto wadogo.

Wakaazi hao wamepinga madai hayo  wakisema kua  mabanda hayo  kamwe hayajaharibu maadili ya watoto ila ni  wazazi wameshindwa kuwatunza wana wao .

Haya yanajiri siku chache tu baada ya kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo kuagiza machifu na manaibu kamishna kuhakikisha mabanda yote ya video ambayo yanaendeshwa bila leseni kufungwa.

Show More

Related Articles