HabariMilele FmSwahili

Spika wa kaunti ya Nairobi Beatrice Elachi abanduliwa afisini

Kizaa zaa kinashuhudiwa katika bunge la kaunti ya Nairobi,waakilishi wadi wakimbandua afisini spika Beatrice Elachi.Wakiongozwa na kiongozi wa wengi Abdi Guyo, waakilishi hao wanadai Elachi hafai kuhudumu kwani walimbandua wiki jana.Polisi wamelazimika kumpa ulinzi Elachi na hata kuwarushia vito machozi waliovamia afisi zake.Waakilishi wadi hao wamepuzulia mbali agizo la mahakama lililomruhusu Elachi kusalia afisini wakilitaja kama lisilo na uzito.Lakini akiongea awali,Elachi anasisitiza vita vyake na waakilishi hao vinatokana na yeye kupambana na ufisadi.Anawashtumu waakilishi hao kwa kukosa heshima kwake huku akiapa kupambana nao kuhakikisha hadhi ya bunge hilo inasalia.

Show More

Related Articles