HabariMilele FmSwahili

Kesi dhidi ya msaidizi wa Obado,Michael Oyamo yahairishwa

Kesi ya mauaji inayomkabili Michael Oyamo mshukiwa katika mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno imeahirishwa. Hakimu Leister Simiyu atatoa uamuzi wake kuhusiana na mawakili wa Oyamo na upane wa mashtaka saa saba mchana huu. Kati ya mengine mawakili wa Oyamo wanawatuhumu maafisa wa polisi kwa kuendesha uchunguzi wa DNA bila kufuata mpangilio wa kisheria. Wanalalamikia pia polisi kumzuilia mshukiwa kwa zaidi ya saa 24 tokea alipokamatwa jumanne iliyopita. Upande wa mashtaka hata hivyo unataka muda zaidi kukamilisha uchunguzi wa DNA na data za mawasiliano za simu ya mshukiwa.

Show More

Related Articles