Mediamax Network Limited

Washukiwa Wa Mauaji Ya Sharon Otieno Wafikishwa Mahakamani.

Washukiwa watatu wa mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo Sharon Otieno wamefikishwa katika mahakama ya Homabay.

Washukiwa hao ni pamoja na msaidizi wa karibu wa gavana Okoth Obado, Michael Oyamo ambaye amekuwa kizuizini tangu wiki jana, na aliyekuwa mwakilishi wadi miongoni mwa mwengine mmoja.

Upande wa mashtaka umeiomba mahakama muda wa siku 10 kukamilisha uchunguzi wao, ombi ambalo limepingwa vikali na upande wa utetezi.

Wakati huo huo mawakili wa utetezi wameiambia mahakama kwamba majasusi walichukua sampuli za DNA za mshukiwa Oyamo akiwa kizuizini kinyume cha sheria.

Mahakama ya Homabay kwa sasa imeahirisha vikao hivyo hadi saa saba adhuhuri ambapo hakimu mkaazi Lesister Simiyu anatarajiwa kutoa uamuzi wake wa iwapo washukiwa hao wataachiliwa kwa dhamana au la na pia uamuzi kuhusiana na ombi la upande wa mashtaka la kutaka muda zaidi.