HabariMilele FmSwahili

Raila aelekea nchini Ghana kuhudhuria mazishi ya Kofi Annan

Kinara wa upinzani Raila Odinga ameondoka nchini usiku wa leo kuelekea nchini Ghana ambako atahudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Dkt Kofi Annan. Spika wa bunge la taifa Justine Muturi atamwakilisha rais Uhuru Kenyatta katika mazishi hayo tarehe 13 mezi huu. Dkt Kofi Annan aliaga dunia Agosti 18 nchini Uswizi akiwa na miaka 80 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Kando na mazishi ya Dkt Annan, Raila pia ameratibiwa kuzuru Marekani ambako atahutubu kwenye vyuo vikuu vya Duke University huko North Carolina na chuo kikuu cha George Washington. Kadhalika Raila atahutubia mkao wa shirika la Council on Foreign Relations kisha akutane na maafisa wa serikali ya Marekani na wafanyibiashara.

Show More

Related Articles