Mediamax Network Limited

Oscar Sudi aitaka DCI kumtia mbaroni gavana Obado kuhusiana na kifo cha Sharon

Mbunge wa Kapseret kaunti ya Uasin Gishu Oscar Sudi ameitaka idara ya dci kumtia mbaroni gavana wa Migori Okoth Obado kuhusiana na kifo cha mwanafunzi Sharon Atieno.Akiongea  katika shule ya msingi ya Langas Sudi amesema gavana huyo amehusishwa pakubwa na mauaji ya mwanafunzi huyo na polisi wanapaswa kuhakikisha gavana huyo anaandikisha taarifa.Sudi amewaonya wanasiasa wanaokuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi wa vyuo vikuu kuwajibika.