HabariPilipili FmPilipili FM News

Zaidi Y Vijana 50 Wameuawa Kwa Kupigwa Risasi Na Maafisa Wa Polisi mwaka huu Katika Kaunti Ya Mombasa

Shirika la haki za binadam la MUHURI na mamlaka ya kuangazia utendakazi wa polisi nchini IPOA ,pamoja na familia za vijana watatu waliopigwa risasi na kuaawa eneo la kisauni hapo jana, sasa wanataka haki ipatikane kwa familia hizo.

Vijana hao ni Kenga Ramadhan mwenye umri wa miaka 19, Juma Kitsao mwenye umri wa miaka 18 na Bilal Masood mwenye umri wa miaka 17.

Inakisiwa tangu mwaka huu wa 2018 ztakriban visa 56 vimeripotiwa vya watu kupigwa risasi kiholela eneo hili la pwani pekee, huku maafisa wa polisi wakinyoshewa kidole cha lawama kutokana na visa hivyo.

Show More

Related Articles