HabariMilele FmSwahili

Bobi Wine aapa kurejea Uganda kupigania haki za wanyonge

Mwanasiasa anayekabiliwa na mashtaka ya uhaini nchini Uganda  Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine ameapa kurejea nchini humo kupigania haki za wanyonge.Bobi Wine ambaye alienda kupata matibabu nchini Marekani kutokana na mateso anayodaiwa kupitia jeshi nchini humo alisimulia machungu aliyo nayo kufuatia kifo cha dereva wake aliyefariki wakati wa vurugu za kisiasa mwezi Agosti.Bobi Wine alisema kuwa figo yake ilijeruhiwa na sehemu zake nyeti wakati alipokamatwa na kupitia mateso mikononi mwa wanajeshi wa Uganda.

Show More

Related Articles