HabariMilele FmSwahili

Hajji amtaka Maraga kubuni kikao cha majaji 5 kusikiliza kesi inayomkabili Mwilu

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Noordin Hajji sasa anamtaka jaji mkuu David Maraga kubuni kikao cha majaji 5 kusikiliza kesi ya ufisadi inayomkabili naibu jaji mkuu Philomena Mwilu. Katika ombi alilowasilisha mahakamani kupitia  kiongozi mkuu wa mashtaka Lilian Ogwora Hajji anasema kesi hiyo inaibua maswala yenye uzito na umuhimu wa kitaifa na sharti isikilizwe na zaidi ya jaji mmoja. Hajji pia anamtaka jaji mkuu kubuni kikao cha majaji hao upesi kabla ya Oktoba 9 ambapo kesi hio imeratibiwa kusikizwa. Jaji Chacha Mwita atatoa uamuzi kuhusu ombi la Hajji.

Show More

Related Articles