Mediamax Network Limited

Watoto 3 wateketea hadi kufa usiku wa kuamkia leo Kitui

Watoto watatu wameteketea hadi kufa usiku wa kuamkia leo baada ya nyumba yao kushika moto kijijini Masasani eneo la Kitui Kusini. Inaarifiwa watoto hao wa miaka 7, 5 na mbili na nusu walikuwa wamefungiwa ndani ya nyumba hiyo na mama yao aliyekuwa amekwenda kupokea mzigo aliotumiwa kutoka hapa jijini Nairobi. Kulingana na chifu wa eneo hilo Christine Kalunda mkasa huo huenda ulitokana na kulipuka taa nyumbani humo. Majirani waliofika katika nyumba hiyo hawakuweza kuokoa chochote. Miili ya watoto hao inahifadhiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ya Mutito.