Mediamax Network Limited

Vijana wahimizwa kukumbatia masomo ya kiufundi

Changamoto inazidi kutolewa kwa vijana  kukumbatia masomo ya kiufundi ili kuchangia kikamilifu katika ujenzi wa taifa. Seneta wa Embu Njeru Ndwiga anasema ni jambo la kutia hofu kuwa taifa kwa sasa linakumbwa na uhaba wa wataalamu wa kiufundi. Akizungumza kaunti yake seneta Ndwiga amewashauri wazazi kuwahimiza wanao wanaokosa nafasi katika vyuo vikuu kijiunga na taasisi za mafunzo ya kiufundi hasaa baada ya serikali kutangaza  ufadhili kwao.