HabariMilele FmSwahili

Mwalimu 1 atiwa nguvuni Nakuru kwa kukosa kuwapeleka wanawe shuleni

Mwalimu mmoja huko Langalanga kaunti ya Nakuru ametiwa nguvuni kwa kukosa kuwaepeleka wanawe shuleni na kuripoti kazini akiwa mlevi.Charles Mukwa mwalimu wa shule ya upili ya Kivumbini, alikamatwa baada ya mkewe kumripoti kwa maafisa wa polisi.Chifu wa eneo hilo George Nganga anasema mwalimu huyo alikuwa mlevi chakari na hakuwa na uwezo wa kuzungumza wakati akikamatwa.Mkewe Teresiah Moraa ambaye wamekuwa pamoja kwa miaka 17 anasema wamekuwa na ugomvi wa kinyumbani kila mara mmewe akija akiwa mlevi.Ameongeza kuwa wanawe watatu hawajakuwa wakihudhuria masomo kutokana na kutolipiwa karo.

Show More

Related Articles