HabariMilele FmSwahili

Mahakama ya Bungoma yasitisha utekelezwaji ushuru wa asilimia 16

Mahakama ya Bungoma imesitisha kwa muda utekelezwaji ushuru wa asilimia 16.Hii ni kufuatia kesi iliyowasilishwa na  wakili Ken Amodi, anayedai ushuru huo unakiuka katiba.Jaji Stephen Riech ameamuru kesi hiyo kutajwa tarehe 12 mwezi huu mjini Kisumu.Hayo yakijiri, usambazaji mafuta utarejelewa kama kawaida kufikia mwisho wa siku.Hakikisho hili limetolewa na shirika la kitaifa la mafuta likisema kiwango kikubwa cha mafuta kimechukuliwa na wasambazaji hivi leo.Uhaba wa mafuta ulikuwa umechangiwa na mgomo wa wasafirishaji mafuta ambao baadhi yao wamerejelea shughuli leo.

Show More

Related Articles