HabariPilipili FmPilipili FM News

Majadiliano Ya Kutafta Suluhu Kuhusu Ongezeko La Bei Ya Mafta Ya n`goa Nan`ga

Waziri wa fedha Henry Rotich hii leo amefanya kikao cha faragha na wadau mbalimbali ikiwemo afisi ya mwanasheria mkuu Paul Kihara, kiongozi wa wengi bungeni Aden Duale, spika wa bunge la seneti Ken Lusaka pamoja na spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi miongoni mwa wengine.

Kulingana na spika Muturi mkao wa leo ulilenga kujadili namna ya kuondoa ushuru wa mafuta unaoendelea kuibua hisia kali miongoni mwa wakenya.

Waziri Rotich amewahakikishia wakenya majadiliano yataendelea hadi mwafaka upatikane ili kuwaondolea wakenya gharama ya juu inayowakumba kwa sasa.

Tayari wasambazaji mafuta wameanza kusambaza mafuta kwa vituo vya mafuta jijini Nairobi ambako awali kumeshuhudiwa msongamano wa magari kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo.

Show More

Related Articles