HabariPilipili FmPilipili FM News

Wasafirishaji Mafuta Waapa Kutositisha Mgomo Wao.

Wasafirishaji mafuta kaunti ya mombasa wameapa kutositisha mgomo wao ulioanza siku ya jumanne, hadi serikali iondoe ushuru wa asilimia 16 unaotozwa bidhaa za mafuta nchini.

Wengi wao wanasema ushuru huo umechangia bei ya mafuta kupanda maradufu kwa kiwango ambacho ni vigumu mwananchi kumudu.

Baadhi ya madereva wa magari ya mafuta wanaitaka serikali kushughulikia hali hiyo haraka wakihofia kukosa ajira, ikizingatiwa tayari wenye magari ya kusafirishia mafuta wameondoa magari yao barabarani.

lita ya mafuta ya petrolI kufikia sasa inauzwa kati ya shilingi 124 na 131 hapa mombasa, ikilinganishwa na bei ya awali ya shilingi 105.

Mafuta ya diseli lita moja kwa sasa inauzwa kati ya shilingi 110 na 117, tofauti na  shilingi 95 hapo awali,  huku  mafuta ya taa lita moja ikiuzwa shilingi 93 na 100, tofauti na shilingi 70 hapo awali.

Show More

Related Articles