HabariMilele FmSwahili

KNUT yatishia hatua kali iwapo TSC haitositisha zoezi la kuwatuma kwengine waalimu

Mgogoro kati ya muungano kati ya muungano wa walimu KNUT na tume ya TSC kuhusu kuwapa uhamisho walimu unazidi kutokota. KNUT imeapa kuchukua hatua ambazo haitaweka bayana iwapo TSC haitabatili agizo lake kwa wanachama wake tawi la Masaba kaunti ya Kisii kuelezea sababu za kudinda kupewa uhamisho. Kulingana na KNUT, TSC imekiuka agizo la rais kusitisha uhamisho wa walimu, walimu 130 wakipewa uhamisho kufikia sasa.Kadhalika katibu mkuu wa KNUT Wilson Sossion amewataja kuwa wanafiki wakuu wa TSC kwa kukana makubaliano yaliyoafikiwa katika mkutano wa pande hizo hivi karibuni. Sossion amesema walimu kamwe hawatatia saini mkataba wa utendakazi. Amedoeza kuwa walimu hawatakuwa na budi ila kugoma iwapo mazungumzo baina ya KNUT na TSC hayatazaa matunda.

Show More

Related Articles