HabariMilele FmSwahili

Shughuli ya upasuaji wa mwili wa marehemu Sharon Otieno yaendelea wakati huu

Shughuli ya upasuaji wa mwili wa marehemu Sharon Otieno mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo aliyepatikana ameuwawa jana ikifanyika wakati huu katika hospitali ya Homabay Level 5. Hayo yanajiri wakati maafisa wa idara ya jinai wakiendelea kuwasaka wahusika wa mauaji hayo. Usimamizi wa chuo kikuu cha Rongo kaunti ya Migori umelaani vikali mauaji ya Sharon, Naibu Chansela Profesa Gudu Lezia akitaka wahusika wa mauaji kukamatwa na kushtakiwa. amesema usimamizi wa chuo pia unashirikiana na jamii ya marehemu katika maandalizi ya mazishi. Profesa Lezia pia amewahakikishia usalama wao wanafunzi katika chuo hicho akisema hawana cha kuhofia.

Show More

Related Articles