HabariMilele FmSwahili

Idara ya uhamiaji kumrejesha kwao raia wa China aliyetoa matusi dhidi ya wakenya

Idara ya uhamiaji wakati wowote itamrejeshwa kwao raia wa China Liu Jiai aliyenaswa kwenye video akitoa matusi dhidi ya wakenya. Idara hiyo inasema jamaa huyo ambaye kwa sasa yuko katika uwanja wa ndege wa Jommo Kenyatta ataondolewa nchini kwa tuhuma za ubaguzi wa rangi. Aidha idara hiyo imedhibitisha kibali chake cha kufanya kazi nchini kimefutiliwa mbali. Hii ni baada ya kunukuliwa kwenye video akimtisha mfanyikazi mkenya katika duka lake la piki piki na kudai wakenya ni nyani.

Show More

Related Articles