HabariMilele FmSwahili

Makamishna 2 wa IEBC watarajiwa kufika mbele ya kamati la bunge

Makamishna wawili wa tume ya uchaguzi IEBC Boya Molu na Abdi Guliye wanatarajiwa kufika mbele ya kamati ya masuala ya haki na sheria bungeni asubuhi hii.Hata hivyo,mwenyekiti Wafula Chebukati hatafika mbele ya kamati hiyo alivyotakiwa kwani bado yuko nchini Rwanda ambapo anafuatalia uchaguzi wa taifa hilo kama mmoja wa waangalizi wakuu.Kamati hiyo yake William Cheptumo inataka kupata majibu mwafaka kutoka kwa wawili hao kuhusiana na mzozo wa uongozi  unaoendelea ndani ya IEBC.Uamuzi wa kuwahoji wakuu hao unafuatia hatua yao kuzima jaribio la  makamishna Paul Kurgat,Margret Mwachanya na Connie Nkatha kurejea afisini miezi minne baada yao kutangaza kujiuzulu.

Show More

Related Articles