Milele Fm

Kajwang’ apendekeza serikali za kaunti kuhusishwa katika masuala ya usalama nchini

Seneta wa Homa Bay Moses Kajwang’ anapendekeza serikali za kaunti kuhusishwa katika masuala ya usalama nchini.Kajwang’ anasema japo idara ya polisi inasalia chini ya uongozi wa serikali kuu,kuna haja ya serikali za kaunti kushirikishwa.Kulingana naye,kila kunapotokea suala la dharura kuhusu usalama wananchi hulaumu magavana bila ufahamu kwamba hawana jukumu lolote ikiwemo kutoa agizo kwa polisi kutoa msaada hitajika.Anasema njia bora kuwashirikisha magavana kwenye masuala ya usalama ni kuwaruhusu kuketi katika mikutano ya kiusalama ambayo ilivyo sasa huongozwa na kamishna wa kaunti.

Show More

Related Articles