HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Kamanda wa Trafiki Samuel Kimaru afichua masaibu yanayomkabili

Kamati ya uchukuzi bungeni chini ya mwenyekiti wake mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing imemuamurisha Inspekta Mkuu wa Polisi Joseph Boinet kufika mbele yake jumatatu saa tano asubuhi.

Hii ni baada ya Kamanda wa Trafiki Samuel Kimaru kuiambia kamati hiyo kwamba hana mamlaka kuendesha maswala ya idara ya trafiki hatua iliyochangia ongezeko la ajali tangu mamlaka ya usafiri na usalama barabarani NTSA kuondoka barabarani.

Show More

Related Articles