Mediamax Network Limited

ERC: Bei ya sasa kusalia, tofauti na msimamo wa wizara ya Kawi

Tume ya kudhibiti kawi, ERC imepinga ombi la wizara ya kawi la hapo jana kwamba wizara ya fedha isitishe kwa muda utekelezaji wa ushuru wa asilimia 16 unaotozwa kwa petroli na mafuta.

ERC inasema kuwa takwimu zilizotolewa ili kufanikisha bei mpya iliyoanza kutekelezwa Septemba mosi ni sawa na hadi uratibu mpya wa bei mnamo Februari 14 bei ya sasa kote nchini itasalia.