HabariMilele FmSwahili

ELOG yataka chaguzi zijazo za viongozi kugawanywa na kuandaliwa siku tofauti

Kundi la waangalizi wa uchaguzi nchini ELOG sasa linataka chaguzi zijazo za viongozi mbali mbali kuwaganywa na  kuandaliwa siku tofauti. Kundi hilo linasema kuandaliwa kwa uchaguzi wa viongozi sita siku moja kumeathiri uwezo wa kuaminika kwa matokeo ya uchaguzi. ELOG linasema uchunguzi wake kuhusiana na usimamizi wa uchaguzi mkuu mwaka jana ulidhihirisha changamoto nyingi zilizokumba IEBC na juhudi za kuandaa uchaguzi huru na wa kuaminika. Kundi hilo pia linataka mageuzi kabambe kuwekwa ili kuzuia visa vya rushwa na uvunjaji sheria wakati wa uchaguzi. Yusuf Nzibo ni mwenyekiti wa SUPKEM na mwanachama wa ELOG.

Show More

Related Articles