HabariMilele FmSwahili

Wabunge wa ODM wawasilisha ombi mbele ya mahakama kusitisha utekelezwaji wa ushuru kwa bidhaa za mafuta

Wabunge wa ODM wamewasilisha ombi mbele  ya mahakama ya Milimani kusitisha utekelezwaji wa ushuru wa asilimia 16 kwa bidhaa za mafuta. Wakiongozwa na Babu Owino wa Embakasi Mashariki, wabunge hao wanasema bei ya mafuta nchini ni ghali mno na hivyo mahakama inafaa kusitisha ili kutafutwa mwafaka wa hali hiyo ,Babu aliyeambatana na Mark Nyamita mbunge wa Uriri katika mahakama hiyo, wamemtaka rais Uhuru Kenyatta kufanya upesi na kutia saini mapendekezo ya bunge kuhairishwa utekelezwaji wa ushuru huo miaka 2 ijayo

Show More

Related Articles