HabariPilipili FmPilipili FM News

Bei Ya Unga Yatarajiwa Kupanda Kutakana Na Gharama Ya Juu Ya Uzalishaji.

Huku wakenya wakiendelea kulalama kuhusu kupanda kwa bei za mafuta, inahofiwa huenda bei za unga wa ngano na mahindi  zikapanda kutokana na ushuru wa asilimia 16 kwa bidhaa za mafuta.

Muungano wa Wasagaji nafaka, CMA umetangaza kuwa bei ya bidhaa hizo itaongezeka kutokana na gharama ya juu ya kuzalisha unga.

Muungano huo aidha unalaumu wizara ya fedha kwa ongezeko la bei za mafuta, ukisema linaathiri wadau wote wa sekta hiyo, wakiwemo wazalishaji wa unga, wanunuzi na hata wasafirishaji.

Kauli ya muungano huo imeungwa mkono na kinara wa chama cha ANC Musalia Mudavadi ambaye sasa anaitaka serikali kutafuta njia mbadala za kuzalisha mapato ya taifa badala ya kuwalimbikizia wakenya mzigo.

Show More

Related Articles