People Daily

Vyama Vya Wafanyikazi Vya Takaka Pia Mishahara Ya Wafanyikazi Iongezwe.

vyama vya wafanyikazi nchini vikiongozwa na COTU vimetishia kuandaa maandamano endapo rais Uhuru Kenyatta atakosa kutia saini mswada uliofanyiwa marekebisho na bunge wiki jana ili kusitisha utekelezwaji wa asilimia 16 ya ushuru kwa bidhaa za mafuta nchini.

Maafisa wakuu wa vyama vya wafanyikazi wanasema endapo ushuru huo utaidhinishwa basi pia mishahara ya wafanyikazi iongezwe kulingana na ugumu wa maisha.

Wakati Uo huo maafisa hao wameeleza kushangazwa na hatua ya serikali kuongeza ushuru kwa bidhaa za mafuta wakati ikiwa bado hata kutekelezwa kwa nyongeza ya mshahara iliyotangazwa na serikali.

Show More

Related Articles