HabariMilele FmSwahili

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo aliyetekwa nyara apatikana amefariki

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo aliyetekwa nyara pamoja na mwanahabari wa shirika la Nation Barack Oduor katika kaunti ya Migori amepatikana amefariki. Mwili wa Sharon Otieno mwanafunzi wa mwaka wa pili katika chuo kikuu cha Rongo ulipatikana msitu wa  Kodera usiku wa kuamkia leo. Mwili huo unahifadhiwa katika chumba cha maiti cha Oyugis Level 4 uchunguzi ukiendelea. Sharon pamoja na Oduor walitekwa nyara kutoka hoteli moja mjini Rongo jumatatu usiku. Oduor alinusurika baada ya kuruka kutoka gari la watekaji nyara hao katika soko la Nyangweso kwenye bara bara ya Hombay Kisumu. Polisi wanamhoji  Michael oyamo msaidizi wa gavana Okoth Obado kuhusiana na tukio hilo.

Show More

Related Articles