HabariPilipili FmPilipili FM News

Vibanda Vya Video Vinavyo Endeshwa Bila Leseni Katika Kaunti Ya Kwale Vya Agizwa Kufungwa.

Kamishna wa kaunti  ya  Kwale  Karuku Ngumo ameagiza kufungwa  kwa  mabanda  ya video yanayoendeshwa  bila vibali  hitajika.

Ngumo  anasema licha ya mabanda hayo kukosa leseni, mengi yako karibu na shule na maakazi ya watu hali inayochangia watoto wengi kukwepa masomo shuleni na kujificha katika mabanda hayo.

Kulingana naye mabanda hayo mara nyengine huonyesha picha za ngono ambazo huchangia kuporomoka maadili ya watoto.

Show More

Related Articles