HabariPilipili FmPilipili FM News

Idara Ya Usalama Yatishia Kupiga Marufuku Sherehe Za Usiku Katika Kaunti Ya Kwale.

Huenda  sherehe za usiku  zikapigwa marufuku kabisa katika kaunti ya kwale.

Idara ya usalama katika kaunti hiyo inasema visa vingi vya uhuni vimekuwa vikishuhudiwa kutokana na sherehe hizo, ikiwemo wizi , ubakaji na hata watoto kutekwa nyara.

Kulingana na Mkuu wa  kituo cha polisi cha Kwale Ludwin Sasati visa hivyo  hutekelezwa  na  vijana  wa umri mdogo, huku maeneo ya Kombani , Ng’ombeni na Lungalunga  yakiathirika zaidi.

Show More

Related Articles