HabariPilipili FmPilipili FM News

Wabunge Kutoka Kaunti Ya Mombasa Waonesha Kutoridhishwa Na Kupanda Kwa Kodi Ya bidhaa Za Petroli.

Wabunge wa kaunti ya Mombasa wamepinga  mswada wa kupandishwa kwa kodi dhidi ya bidhaa za mafuta ya petroli nchini.

Wakiongozwa na mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir , mbunge wa Nyali Mohammed Ali na Mishi Mboko wa likoni wamemwomba Rais Kenyatta kutia saini mswada uliofanyiwa marekebisho na bunge kuwa sheria ili kuwaondolea wakenya gharama.

Mbunge wa Mvita Shariff Nassir amesema bei ya mafuta ikipanda basi kila kitu kitapanda bei, na hivyo kumgandamiza mwananchi wa kawaida.

Show More

Related Articles