HabariMilele FmSwahili

Idara ya polisi yapokea magari 800 kutoka kwa kampuni ya Toyota

Idara ya polisi imepigwa jeki baada ya kupokea magari 800 kutoka kwa kampuni ya toyota chini ya mpango wa serikali kukodisha magari hayo. Magari hayo yatakayotolewa kwa muda wa wiki 2 zijazo yataimarisha utendakazi wa maafisa wa polisi nchini. Mkurugenzi wa  Toyota Kenya Arvinder Reel anasema maafisa wa polisi 2,500 watapokea mafunzo jinsi ya kuyatumia magari hayo katika kaunti 41. Takwimu zinaonyesha kwa sasa,idara ya polisi inahitaji magari 4,500 zaidi huku hitaji hilo likitarajiwa kuongezeka hadi magari 11,000 kwa muda wa miaka mitano ijayo.

Show More

Related Articles