HabariMilele FmSwahili

Moto kubwa wateketeza bweni la shule ya upili ya Senior Chief Koinange Kiambu

Mali ya dhamani isiyojulikana imeharibika baada ya moto mkubwa kuteketeza bweni la shule ya upili ya wasichana ya Senior Chief Koinange kaunti ya Kiambu. Polisi wamedhibitisha kuwa hakuna aliyejeruhiwa kwenye mkasa huo wa saa 11 asubuhi hii. Wenye walishirikiana na zima moto kutoka serikali ya kaunti ya Kiambu kudhibiti mikasa huo. Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo chake huku baadhi ya wakazi wakidai huenda moto huo uliwashwa na baadhi ya wanafunzi.

Show More

Related Articles