HabariMilele FmSwahili

Afisa 1 wa polisi anusurika kifo baada ya kuanguka kwenye shimo lenye urefu wa futi 60 Bomet

Afisa mmoja wa polisi wa utawala amenusurika kifo baada ya kuanguka kwenye shimo lenye urefu wa futi 60 eneo la Kembu, kaunti ya Bomet. Afisa huyo aliyekesha shimoni alinusuriwa na wananchi  chifu wa eneo hilo Daniel Tuiyo anasema mwathiriwa alikuwa akitembea vichochoroni alipotumbukia shimoni. Tuiyo aidha amewataka wenyeji kufunika mashimo yote yaliyo wazi ili kuepusha mikasa.

Show More

Related Articles