HabariK24 TvSwahiliSwahili VideosVideos

Wavuvi wa Kenya hawatanyanyaswa na askari wa Uganda, Ziwa Victoria

Ni afueni kwa wavuvi katika Ziwa Victoria baada ya Waziri wa Usalama Fred Matiang’i kusema kwamba visa vya unyanyasaji chini ya maafisa wa usalama kutoka nchi jirani ya Uganda vitakoma mara moja.

Matiang’i kwenye mkutano na wakuu wa usalama eneo la Nyanza na Magharibi mwa Kenya amesema  tayari makubaliano baina ya serikali ya mataifa hayo mawili yametiwa sahihi.

Aidha Matiang’i ameonya dhidi ya ongezeko la wafanyikazi wa kigeni wanaoendeleza biashara haramu humu nchini.

Show More

Related Articles