HabariPilipili FmPilipili FM News

Vijana Waombwa Kujiandikisha Kama Makundi Ya Kibiashara Ili Kupokea Mikopo kutoka kwa Hazina Ya Vijana

Imebainika kuwa kaunti ya Mombasa ndiyo ina idadi ndogo ya vijana wanaochukua mikopo kutoka kwa hazina ya vijana nchini almaarufu Youth Enterprise Development Fund.

Haya ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa hazina hiyo Ronald Osumba ambaye amesema kwa muda wa miaka 10, vijana wa kaunti ya Mombasa wamechukua shilingi milioni 87 pekee na vile vile mikopo hiyo imelipwa kwa asilimia 67 ambayo ni chini ya asilimia 84 inayotarajiwa.

Amesema haya katika hafla ya sherehe za kuhitimu kwa vijana 120 waliokuwa wakipitia mafunzo ya upakaji rangi ambayo yalisimamiwa na kampuni ya Rangi Africa.

Vile vile, ameahidi kupeana mkopo wa shilingi milioni 2.4 kutoka kwa hazina hiyo kwa vijana hao punde watakapojiandikisha kama makundi ya kibiashara.

Kampuni ya Rangi Africa imeweka kando kiasi cha milioni 8 kwa mradi wa kufunza vijana upigaji rangi katika mji wa Mombasa utakaofanyika kwa muda wa mwaka mmoja.

Show More

Related Articles