HabariPilipili FmPilipili FM News

KRA Ya Apa Kukabiliana Vilivyo Na Wale Wanaoingiza Bidhaa Ghushi Hapa Nchi.

Siku chache baada Rais Uhuru Kenyatta kuongoza zoezi la kuharibu mali ghushi yenye thamani ya shilingi bilioni 7.4 zilizo naswa nchini kinyume cha sheria, mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini KRA inasema sasa itakabiliana vikali na wale wanaoingiza bidhaa ghushi nchini.

Kamishna mkuu wa mamlaka hiyo John Njiraini anasemawanaweka mikakati mipya, ambapo kuanzia tarehe 15 mwezi huu wa sweptemba bidhaa zote zinazoingia nchini zitakuwa zinakaguliwa katika nchi zinakotoka kabla ya kusafirishwa nchini.

Njiraini amelaumu kampuni za kukagua ubora wa bidhaa kwa kuzembea katika mchakato wa ukaguzi hali inayochangia kuingizwa kwa bidhaa ghushi humu nchini

Show More

Related Articles