HabariPilipili FmPilipili FM News

Wambunge Wamtaka Rais Uhuru Kuidhinisha Sheria Ya Utekelezaji Wa asilimia 16 ya Ushuru Wa Bidhaa Za Petroli

Wabunge sasa wanamtaka rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati na kutia saini kuwa sheria mswada uliopitishwa na wabunge wiki jana,  ili  kusitisha utekelezwaji wa asilimia 16 ya ushuru wa bidhaa za petroli.

Mbunge wa rabai kaunti ya kilifi WILLIAM KAMOTI amemkosoa waziri wa fedha Henry Rotich kwa kuidhinisha sheria hiyo tata , akimtaka kuiondoa na kupendekeza njia mbadala za kuzalisha mapato ya taifa, ili kuwaondolea wakenya gharama ya maisha.

Serikali inapania kukusanya ushuru wa kima cha shilingi bilioni 70 ili kujazilia fedha za kufadhili miradi na kulipa deni la taifa.

Show More

Related Articles