HabariPilipili FmPilipili FM News

Nauli Ya BodaBoda Yaongezeka kwa Shilingi Ishirni Katika Kaunti Ya Mombasa.

Nauli Ya BodaBoda Yaongezeka kwa Shilingi Ishirni Katika Kaunti Ya Mombasa.

Wakazi wa Mombasa wanaotumia uchukuzi wa bodaboda watalazimika kulipa shilingi 20 zaidi juu ya nauli za awali.

Katika baadhi ya vituo tayari wahudumu wa sekta hiyo wameweka notisi ya ongezeko hilo  kutokana na kupanda kwa bei za mafuta.

Kufikia sasa lita moja ya mafuta ya petrol inauzwa kwa shilingi 124 hapa mombasa, ikilinganishwa na bei ya awali ambayo ilikuwa shilingi 105.

Mafuta ya diseli lita moja kwa sasa inauzwa kwa shilingi 110 tofauti na  awali ambapo iliuzwa kwa shilingi 95,  huku  mafuta ya taa ikiuzwa shilingi 93 kwa lita, tofauti na bei ya awali ya  shilingi 70.

Ongezeko hilo linajiri baada ya Mamlaka ya Kodi nchini KRA kutangaza kuidhinisha  utekelezwaji wa ushuru wa asilimia 16 kwa bidhaa za mafuta , hata licha ya bunge kutaka sheria hiyo iahirishwe kwa miaka miwili.

Show More

Related Articles