HabariMilele FmSwahili

LSK yapongeza juhudi za Noordin Hajji kuwakabili washukiwa wa ufisadi

Chama cha mawakili  nchini LSK kimepongeza juhudi za mkurugenzi wa mashtaka Noordin Hajji kuwakabili washukiwa wa ufisadi.Akizungumzia kesi ya ufisadi inayomkabili naibu jaji mkuu Philomena Mwilu rais wa LSK Allen Gichuhi anasema vita dhidi ya ufisadi vimechukua mwelekeo ufaao chini ya uongozi wa Hajji hali anayosema inafaa kuungwa mkono na wakenya wote. Akizungumza na Milele FM kwa njia ya simu Gichui hata hivyo ametoa changamoto kwa Hajji kukusanya ushahidi wa kutosha ili kuhakikisha kuwa kesi anazowasilisha mahakamani hazitupiliwi  mbali.

Show More

Related Articles