HabariK24 TvSwahiliVideos

Kutana na Mwanamume anayebugia mayai 7 na makaka yake

Githuria

Ni bayana kwamba mtu anaweza kula matunda kama vile maembe pamoja na maganda yake—lakini je mtazamaji, umeshawahi kusikia mtu anayekula mayai pamoja na makaka yake?

Jamaa mmoja, dereva wa matatu eneo la Githurai amekuwa akifanya hivyo kwa zaidi ya miaka minane sasa na kusema hakuna chakula kingine kitamu zaidi kuliko mayai na makaka yake.

Mwanahabari wetu Shukri Wachu alikutana na Issac Nyamwau na kung’amua ni kwa nini jamaa huyu asiye wa kawaida angependa kuorodheshwa kwenye kurasa za kitabu cha World Guiness record.

 

Show More

Related Articles