HabariPilipili FmPilipili FM News

Wahudumu Wa Matatu Waitaka Serikali Kutatua Swala La Ongezeko La Bei Ya Mafuta.

Madereza wa matatu za umma kutoka Mombasa kuelekea Malindi wanasema nauli ya magari itasalia kama kawaida hadi pale watakapopata mwelekeo kamili kutoka kwa wakuu wa SACCO zao.

Hii ni baada ya ripoti kutolewa kuwa bei ya mafutaa ya gari yaweza kuongezeka kuanzia kesho licha ya bunge kutaka serikali kusitisha utekelezaji wa ushuru wa asilimia 16 kwa biadhaa za petroli hadi wakubaliane kuhusu ongezeko hilo.

Aidha wametaka serikali kutatua shida ya ongezeko la bei ya mafuta kwani inaathiri pakubwa uendashaji wa biashara zao.

Haya ni baada ya bunge kupitisha hoja ya kuondoa utekelezwaji huo wa ushuru hadi baada ya miaka miwili kufuatia kupanda kwa gharama ya maisha.

Show More

Related Articles