HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta kuelekea China kwenye kongamano la ushirikiano baina ya Afrika na China

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuelekea Beijing, China ambako ataandaa mazungumzo na viongozi wa kuu wa taifa hilo kwenye kongamano linalohusu ushirikiano baina ya Afrika na China.Kuu katika agenda itakuwa kusaini mkopo wa shilingi bilioni 380 kufadhili awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kutoka Naivasha kuelekea Kisumu.Ziara ya rais inawadia baada ya kuandaa mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ambaye alizuru Kenya, na rais Donald Trump huko Marekani.Rais amesisitiza ziara yake China kamwe haitaathiri ushirikiano baina ya Kenya na mataifa hayo mawili.

Show More

Related Articles