HabariPilipili FmPilipili FM News

Idara Ya Polisi Mjini Voi Yaanzisha Msako Dhidi Ya Watu Walio Hapa Nchini Kinyume Cha Sheria

Polisi mjini Voi kaunti ya Taita Taveta wanaendeleza zoezi la kukagua vibali vya watu  wanaodaiwa kuwa wageni kutoka nje ya nchi.

Ocpd wa Voi Joseph Chesire amesema tayari polisi wamewanasa watu  kupitia operesheni inayoendelea kote nchini ya kutambua uhalali wa raia wageni wanaoishi nchini sawa na kuwanasa waliokiuka sheria kwa kughushi stakabadhi.
Chesire amesema wageni watakaopatikana humu nchini kinyume cha sheria wataregeshwa kwao,na ni sharti wanaotaka kuingia humu nchini kufuata sheria kikamilifu kwa kupata vibali hitajika halali ili kumruhusiwa kuwa nchini.

Show More

Related Articles