HabariPilipili FmPilipili FM News

Miji Ya Mombasa, Malindi Na Lamu Kunufaika Na Viwanda Vya Kusaga Samaki.

Miji ya Mombasa, Malindi Na Lamu ndiyo itakayowekezwa viwanda vikuu vya serikali vya kusaga samaki  wa baharini, huku chuo kikuu cha bandari  kikitakiwa kuja na mtaala mpya wa  kutoa mafunzo ya uvuvi kwa vijana.

Waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri anasema kenya imekuwa ikipoteza mabilioni ya fedha kutokana na kukosekana wavuvi walio na ujuzi wa kuvua samaki katika maji makuu.

Kiunjuri anasema serikali itatoa zaidi ya miche milioni moja  na nusu  ya mikorosho na minazi,  kwa wakulima wa pwani pamoja na  mbegu zenye uwezo wa kutoa mazao kwa haraka.

Show More

Related Articles